JUHUDI ZA PAMOJA ZINAHITAJIKA,TUWE NA SUKARI YA KUTOSHA NCHINI

Sukari ni kiungo muhimu katika vyakula na vinywaji tunavyotumia kila siku,bila shaka tangu ulipoamka asubuhi mpaka muda huu unaposoma makala hii,ulimi wako umeonja ladha ya sukari.

Chakula ulichokula au kinywaji ulichokunywa kinaweza kikawa kimetayarishwa nyumbani kwako au kiwandani. Hii ina maanisha sukari huitajika kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na viwandani.
Mahitaji ya sukari kwa matumizi ya nyumbani ni tani 420,000.
Mahitaji ya sukari kwa matumizi ya viwandani ni tani 170,000.



UZALISHAJI WA SUKARI
Viwanda vya ndani ya nchi vimekuwa vikizalisha kwa wastani wa tani 300,000 za sukari kwa ajili ya matumizi ya nyumbani


Licha ya uzalishaji huo wa sukari,bado kuna upungufu wa sukari nchini,takwimu zina onyesha ya kwamba mwaka 2011/12 kulikuwa na upungufu wa sukari zaidi ya mwaka 2010/11 na 2012/13.


MKASA WA SUKARI-2016
Tangu februari 2016,sukari imeadimika katika maeneo mbalimbali nchini,watu tofauti wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya kuadimika kwa sukari.Baadhi ya watu wanaona kuadimika kwa sukari kunatokana na baadhi ya wafanya biashara kuficha sukari,na watu wengine wanahusianisha uhaba wa sukari na baadhi ya viwanda vya ndani vya kuzalisha sukari kuwa katika msimu wa kutengeneza mitambo ya kuzalisha sukari katika viwanda vyao






Baada ya sukari kukamatwa ilikuja kugundulika ya kwamba sukari hiyo iliingia nchini kiahalali. Uthibitisho huo ulitolewa na TRA.